Matthew 8:1-4

Isa Amtakasa Mwenye Ukoma

(Marko 1:40-45; Luka 5:12-16)

1Isa aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata. 2 aMtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, “Bwana, kama ukitaka, unaweza kunitakasa.”

3Isa akanyoosha mkono wake akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Mara yule mtu akatakasika ukoma wake. 4 bKisha Isa akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Musa, ili kuwa ushuhuda kwao.”

Isa Amponya Mtumishi Wa Jemadari

(Luka 7:1-10)

Copyright information for SwhKC